Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 08:31

Hillary na Trump waonyesha dalili za ushindi kwenye uchaguzi wa 'Super Tuesday'


Donald Trump na Hillary Clinton.
Donald Trump na Hillary Clinton.

Kufikia Jumatano asubuhi mgombea mtarajiwa wa urais kwa chama cha Demokrat Hillary Clinton alikuwa anongoza kwenye majimbo 5 muhimu ya kusini mwa Marekani kulingana na udadisi wa wanahabari akiwa mbele ya mpinzani wake Bernie Sanders kwenye uchaguzi wa awali maarufu kama wa SuperTuesday.

Tayari Clinton anaelezewa kushinda katika majimbo ya Tennessee, Alabama, Georgia, Arkansas, Texas na Virginia. Sanders kwa upande wake ameonyesha ushindi katika jimbo lake la Vermont na pia Massachusetts.

Kwa upande wa chama cha Repablikan, mfanya biashara Donald Trump ameshinda katika Jimbo la Georgia, Alabama, Tennessee, Virginia na Massachusetts.

Ingawaje siku hii maarufu kama SuperTuesday ni muhimu sana katika uchaguzi wa Rais hapa Marekani, baada ya hapa, wagombea wote wangali wana kibarua kigumu. Katika mwezi huu wa Machi pekee, chaguzi 26 za mapema zitafanyika.

Wademokrat watakuwa wakitafuta wajumbe katika majimbo ya Kansas, Lousiana huku wademokrat wakielekea Nebraska baadae wakati waripablikan wakielekea Kentucky na Maine. Jimbo linaloangaliwa kwa makini ni Lousiana ambapo warepublican wanatarajia wajumbe 46 huku wademokrat wakishindania wajumbe 59.

XS
SM
MD
LG