Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:50

Marekani yaitaka Sudan kuchukua hatua za ziada


Wafanyabiashara wakisubiri wateja katika soko mmoja mjini Khartoum, Sudan Novemba 11, 2017.
Wafanyabiashara wakisubiri wateja katika soko mmoja mjini Khartoum, Sudan Novemba 11, 2017.

Miezi mitano baada ya Marekani kuondosha vikwazo, Sudan imetakiwa kuchukua hatua za ziada ili kurejesha mahusiano yake na kuboresha taswira ya nchi hiyo kiuchumi, wataalamu wamesema.

Mnamo mwaka 2017, Marekani iliondosha vikwazo vya kiuchumi vya muda mrefu vilivyokuwa vimewekwa dhidi ya Sudan.

Vikwazo hivyo vilijumuisha katazo la biashara, kukamatwa kwa baadhi ya rasilimali za serikali ya Sudan, na vikwazo dhidi ya mabenki ya Sudan na shinikizo la benki za kigeni kutofanya biashara na Sudan.

Lakini badala ya kuchochea uchumi huo, kuondoshwa kwa vikwazo hivyo vimeainisha hatua mbalimbali za ziada ambazo Sudan lazima izichukue kurejesha mahusiano yake na Marekani.

Kwa miongo mingi, Sudan na Marekani zimekuwa katika mvutano zaidi kuliko ushirikiano. Udhaifu uliyotajwa ni pamoja na kitendo cha kuuwawa kwa balozi wa Marekani mjini Khartoum mwaka 1973, kitendo cha Sudan kumpokea Osama bin Laden katika miaka ya 90 na serikali ya Sudan kuendelea kuunga mkono uvunjifu wa amani dhidi ya raia wa Darfur, jambo ambalo lilitajwa kama mauaji ya halaiki.

Vikwazo vya kwanza kati ya vile ambavyo vimeondoshwa vilikuwa vimewekwa na Rais Bill Clinton mwaka 1997 kutokana na madai ya kuwa Sudan ilihusika na kufadhili ugaidi na rikodi mbaya ya haki za binadamu.

XS
SM
MD
LG