Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 15:56

Sudan yapata waziri mpya wa fedha


Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok

Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok amemteua aliekuwa kiongozi wa kundi la uasi la Darfur Jibril Ibrahim kuwa waziri wa fedha baada ya kufanya mabadiliko  kwenye baraza la mawaziri yaliotangazwa Jumatatu. 

Mabadiliko hayo yamefanyika wakati Hamdock akijaribu kusukuma mageuzi na kupata ufadhili wa kigeni ambao ni muhimu sana katika kupunguza matatizo ya kiuchumi pamoj na kuboresha kipindi cha mpito cha demokrasia nchini Sudan.

Hamdock ambaye alichaguliwa baada ya makubaliano ya kuunda serikali ya mpito ya kijeshi na raiya baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa muda mrefu Omar al Bashir.

Hamdock anadaiwa kuteuwa mawaziri wenye utaalam swala ambalo linasemekana kuwakasirisha wanajeshi. Tangu Julai mwaka uliopita, nafasi 7 za uwaziri zimekuwa zikishikiliwa na makaimu ikiwemo wizara ya fedha.

Baraza jipya lenye mawaziri wengi ni kufuatia mkataba wa Oktoba kati ya serikali na baadhi ya makundi ya uasi. Mkataba huo ulifanywa kwa lengo la kumaliza ghasia kwenye eneo la Darfur na kusini mwa Sudan.

Imetayarishwa na Harrison Kamau

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG