Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 10:16

Sudan yaondoa hali ya dharura.


Muandamanaji akibeba bendera ya Sudan kando ya matairi yanayowaka moto barabarani Khartoum
Muandamanaji akibeba bendera ya Sudan kando ya matairi yanayowaka moto barabarani Khartoum

Serikali ya kijeshi ya Sudan imeondoa hali ya dharura ambayo iliwekwa baada ya kuchukua madaraka kwa njia ya mapinduzi miezi sita iliyopita. Baraza la usalama na ulinzi linalotawala limesema uamuzi huo ulitolewa katika mkutano ulioongozwa na kiongozi wa kijeshi , generali Abdel Fattah al- Burhan.

Serikali ya kijeshi ya Sudan imeondoa hali ya dharura ambayo iliwekwa baada ya kuchukua madaraka kwa njia ya mapinduzi miezi sita iliyopita.

Baraza la usalama na ulinzi linalotawala limesema uamuzi huo ulitolewa katika mkutano ulioongozwa na kiongozi wa kijeshi , generali Abdel Fattah al- Burhan.

Limesema hatua hiyo ina lengo la kutengeneza mazingira ya majadiliano. Maandamano dhidi ya serikali ya kijeshi yameendelea tangu mapinduzi ya mwezi Octoba.

Mapigano baina ya polisi yameuwa takriban watu 100 tangu wakati huo. Katika siku za karibuni vikosi vimewakamata waandamanaji wengi , vikilenga viongozi katika makundi pinzani.

XS
SM
MD
LG