Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:16

Sudan yamrejesha balozi wake kutoka Ethiopia


Waziri Mkuu wa Sudan Abdullah Hamdok
Waziri Mkuu wa Sudan Abdullah Hamdok

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesema mapema Jumatano kuwa serikali imemuita balozi wake alioko Ethiopia wakati hali ya taharuki ikiendelea kupanda kati ya mataifa hayo jirani.

Baadhi ya masuala yanayo zozaniwa ni ghasia za mpakani pamoja na mradi wa bwawa kubwa la maji lililojengwa na Ethiopia kwenye mto wa Blue Nile.

FILE - Julai 20, 2020, Picha kwa hisani ya Adwa Pictures, Bwawa la Umeme la Mto Blue Nile, Guba, Kaskazini Magharibi ya Ethiopia.
FILE - Julai 20, 2020, Picha kwa hisani ya Adwa Pictures, Bwawa la Umeme la Mto Blue Nile, Guba, Kaskazini Magharibi ya Ethiopia.

Msemaji wa wizara hiyo Mansour Boulad ameliambia shirika la habari la AP kwamba mwanadiplomasia huyo atarejea nchini humo baada ya mashauriano ya kidiplomasia kufanyika.

Jumapili iliopita, Khartoum ilidai kuwa Ethiopia iliruhusu wanajeshi wake kuingia kwenye eneo lake, hatua iliotajwa kuwa ya kichokozi. Mwezi uliopita, Ethiopia pia ilidai kuwa wanajeshi wa Sudan walivuka mpaka na kuingia kwenye eneo lake.

XS
SM
MD
LG