Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 30, 2022 Local time: 07:25

Sudan yadai wanajeshi wake wameuwawa Addis Ababa, Ethiopia


Mto Tekeze ulioko kwenye mpaka wa Sudan na Ethiopia

Msemaji wa jeshi la Sudan Nabil Abdullah amesema Jumatatu kupitia ujumbe wa video kwamba jeshi la Ethiopia limeua wanajeshi 7 wa Sudan pamoja na raia mmoja waliokuwa wameshikiliwa mjini Addis Ababa.

Taarifa hiyo ndiyo ya karibuni zaidi inayoashiria kudorora kwa uhusiano kati ya mataifa hayo mawili. Abdullah ametaja mauaji hayo kutekelezwa na waoga, akiongeza kwamba Khartoum itajibu vilivyo.

Taarifa hiyo hata hivyo haijatoa maelezo ya kina kuhusu watu waliouwawa wala kusema walivyojipata mikononi mwa jeshi la Ethiopia. Uhusiano kati ya Ethiopia na Sudan umekuwa ukiyumba katika miaka ya karibuni kutokana na mzozo wa mpakani kuhusiana na ardhi ya ukulima kwenye eneo na al Fashaqa.

Sudan inadai eneo hilo kuwa lake kwa mujibu wa mkataba uliotiwa saini mwanzoni mwa miaka ya 90. Kumekuwa na mapigano ya mara kwa mara katika kipindi cha miaka miwili iliyopita baada ya Sudan kudai kuchukua sehemu kubwa ya eneo hilo na kuomba Ethiopia kuondoa wanajeshi wake kwenye angalao maeneo mawili yanayodaiwa kuwa ndani ya Sudan.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG