Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 20:25

Rais Bashir ateuwa waziri mpya wa ulinzi


Rais wa Sudan, Omar al-Bashir
Rais wa Sudan, Omar al-Bashir

Rais wa Sudan Omar al-Bashir Jumapili alimteua waziri mpya wa ulinzi. Shirika la habari la serikali, SUNA lilisema kuwa bwana Bashir alimteuwa Luteni Jenerali Awad Mohamed Ahmed bin Awaf kuwa waziri wa ulinzi wa nchi hiyo. Luteni Jenerali Awaf aliwahi kuwa mkuu wa ujasusi katika jeshi la Sudan na pia alishikilia wadhifa wa kidiplomasia huko Oman baada ya kustaafu kutoka jeshini miaka kadhaa iliyopita.

Rais Bashir ambaye anatafutwa na mahakama ya kimataif ya uhalifu-ICC kutokana na tuhuma za mauaji ya halaiki huko Darfur magharibi alishinda kwenye uchaguzi mkuu wa urais uliofanyika mwezi Aprili kwa zaidi ya asilimia 94 ya kura ingawaje uchaguzi huo ulisusiwa na vyama vikuu vya upinzani.

Kiongozi huyo alitangaza baraza jipya la mawaziri mwezi Juni wakati waziri wa muda alipochukua wadhifa kutoka kwa Adelrahim Mohamed Hussein ambaye pia anakabiliwa na mashitaka kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu kutokana na mzozo huo wa Darfur.

XS
SM
MD
LG