Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:29

Sudan na Sudan Kusini watupiana lawama baada ya mapambano.


Rais wa Sudan IOmar Al Bashir wakati wa mahojiano na televisheni ya taifa ya nchi hiyo.
Rais wa Sudan IOmar Al Bashir wakati wa mahojiano na televisheni ya taifa ya nchi hiyo.

Sudan kusini yalaumu mashambulizi ya anga kwenye eneo la mafuta ndege za kijeshi za Antonov zimeangusha mabomu Jumanne.

Sudan kusini inailaumu Sudan kwa mashambulizi ya anga ya siku ya pili kwenye eneo lenye utajiri wa mafuta kwenye mpaka ulio na mzozo, siku moja baada ya mapambano ya kijeshi kati ya mahasimu hao wawili.

Waziri wa habari wa Sudan Kusini Gideon Gatpan amesema ndege za kijeshi za kaskazini aina ya Antonov ziliangusha mabomu mawili mapema Jumanne kwenye visima vya mafuta katika jimbo la kusini la Unity.

Ghasia hizo zimekuja siku moja baada ya pande zote mbili kushutumu wanajeshi wa mwenzake kuvuka mpaka , ulio na alama dhaifu unaotenganisha nchi hizo mbili. Pande zote mbili zilidai zinafanya hivyo kujilinda na kujitanganzia ushindi baada ya mapigano. Idadi ya waliojeruhiwa haijulikani.

Baada ya mapambano hayo Jumatatu Rais wa Sudan Omar Al Bashir alitangaza kusimamisha mkutano wa Aprili 3 na mwenzake wa Sudan Kusini Salva Kiir ambao ulikuwa umepangwa kujadili mizozo kuhusu mipaka na mapato ya mafuta.

XS
SM
MD
LG