Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 01:12

Sudan: Maelfu ya kondoo wafariki baada ya meli iliyokuwa inawasafirisha Saudia kuzama


Ramani ya Sudan
Ramani ya Sudan

Meli iliyojaa maelfu ya kondoo ilizama Jumapili katika bandari ya bahari ya Sham ya Suakin nchini Sudan, na kusababisha vifo vya wanyama wengi waliokuwa ndani, lakini wafanyakazi wote walinusurika, maafisa wamesema.

Meli hiyo ya mifugo ilikuwa inasafirisha wanyama hao kutoka Sudan kuelekea Saudi Arabia wakati ilipozama baada ya maelfu kadhaa ya wanyama zaidi kupakiwa ndani ya meli hiyo kuliko kiwango ilichotakiwa kubeba.

"Meli hiyo, Badr 1, ilizama mapema Jumapili asubuhi, afisa wa juu kwenye bandari amesema, akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina.

"Ilikuwa imebeba kondoo 15,800, ambayo ni zaidi ya uwezo wake wa kupakia mizigo."

Afisa huyo amesema meli hiyo ilikuwa inatakiwa kubeba kondoo 9,000 pekee.

Afisa mwingine, ambaye alisema wafanyakazi wote waliokolewa, ameelezea wasiwasi juu ya athari za kiuchumi na kimazingira za ajali hiyo.

"Meli hiyo iliyozama itaathiri shuguli za bandari," amesema.

Ameongeza kuwa "huwenda ikasababisha pia athari za kimazingira kutokana na idadi kubwa ya wanyama waliokufa ambao walikuwa wamebebwa na meli hiyo."

Omar al-Khalifa, mkuu wa chama cha kitaifa cha wanaosafirisha bidhaa nje, alisema meli hiyo ilifanya saa kadhaa kabla ya kuzama, ikimaanisha kuwa ingeweza kuokolewa.

Thamani ya jumla ya mifugo iliyoteketea ni takriban riyal za Saudia milioni 14, sawa na dola za Marekani milioni 4 , amesema Saleh Selim, mkuu wa kitengo cha mifugo kwenye chama hicho, akithibitisha pia kwamba kondoo hao walipakiwa kwenye meli hiyo katika bandari ya Suakin.

Amesema wenye mifugo walipata kondoo 700 pekee, lakini walikutwa wameumia sana na hawatarajii kwamba wataishi muda mrefu.

Selim ameomba uchunguzi ufanyike juu ya tukio hilo.

XS
SM
MD
LG