Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 00:03

Sudan kusini yawa mwanachama wa UN


Mtu akipeperusha bendera ya Sudan Kusini wakati wa sherehe za uhuru mjini Juba, July 9, 2011
Mtu akipeperusha bendera ya Sudan Kusini wakati wa sherehe za uhuru mjini Juba, July 9, 2011

Baraza kuu la umoja wa mataifa limeipa Sudan kusini uanachama wa umoja wa mataifa kuanzia julai 14

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Alhamisi limeipa uanachama Sudan kusini baada ya kupata pendekezo kutoka katika Baraza la Usalama la UN. Nchi hiyo ilijetenga rasmi na kuwa huru julai 9.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilipitisha azimio hilo Jumatano likipendekeza uanachama wa Sudan Kusini kwenye Umoja wa mataifa. Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon aliliambia baraza hilo kuwa kama mtoto anayezaliwa Sudan Kusini inahitaji msaada. Alitaja tume ya umoja wa mataifa huko Darfur , kuondoka kwa tume ya umoja wa mataifa huko Darfur, kupeleka walinda amani katika eneo la mpaka la Abyei na hali katika eneo la Sudan la Kordofan Kusini.

Matamshi katika baraza la usalama kutoka kwa wasemaji wa Sudan Kusini na Sudan yalisisitiza urafiki na si uadui. Makamu rais wa Sudan Kusini Riek Machar alielelezea furaha kubwa ya Sudan kusini kwa hatua ya baraza la usalama.

“Ni imani yetu kuwa tutapatia ufumbuzi masuala yote yaliobaki kati ya kusini na kaskazini kwa njia za amani.”

Amani na usalama alisema Machar. Tunaahidi kufanyankazi kumaliza tofauti zetu kwa mazungumzo na moyo wa ushirikiano. wakati wa sherehe za uhuru wake baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa walisema rais wa Sudan kusini Salva Kiir atakabiliwa na changamoto kubwa ya kubadilisha taifa hilo kutoka kwenye sura ya vita na kuwa huru.

​
XS
SM
MD
LG