Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:05

Sudan Kusini yaunda jeshi linalojumuisha pande hasimu.


Rais wa Sudan Salva Kiir na kiongozi wa upizani Riek Machar ambaye ni Makamu rais, wakipongezana baada ya kuapishwa mjini Juba, Februari 22, 2020. Picha ya AP,
Rais wa Sudan Salva Kiir na kiongozi wa upizani Riek Machar ambaye ni Makamu rais, wakipongezana baada ya kuapishwa mjini Juba, Februari 22, 2020. Picha ya AP,

Serikali ya Sudan Kusini Jumanne imetangaza kuundwa kwa uongozi wa jeshi lililoungana, ikitekeleza kipengele muhimu cha makubaliano ya amani ya mwaka 2018 ambayo wafuatiliaji wanatumai yataisaidia nchi hiyo kupata afueni baada ya miaka kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Taifa hilo changa duniani lilipata changamoto kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mitano kati ya majeshi tiifu kwa Rais Salva Kiir na hasimu wake, Makamu rais Riek Machar, vita ambavyo vilisababisha vifo vya watu 400,000 kabla ya wawili hao kukubaliana kusitisha mapigano mwaka wa 2018.

Tangu wakati huo, kuzuka kwa ghasia za mara kwa mara kulileta hofu kwamba nchi hiyo itarejea kwenye mgogoro, kwa sababu pande hizo mbili zilishindwa kuafikiana kuhusu masuala nyeti ikiwemo kuunganisha majeshi yao, kipengele muhimu cha mkataba wa 2018.

Lakini mapema mwezi huu, Kiir na Machar walifikia mkataba wa kugawana madaraka katika nyadhifa muhimu kwenye vyombo vya usalama, wakikubaliana kwamba upande wa Kiir utapata asilimia 60 ya nyadhifa hizo za uongozi katika jeshi, polisi na idara za kitaifa za usalama, huku upande wa Machar ukipewa asilimia 40.

Jumanne jioni, radio ya taifa SSBC imesoma mfululizo wa amri za rais zinazotangaza uamuzi wa Kiir kuwateua wajumbe wa chama cha upinzani cha Machar, Sudan People’s Liberation Movement kuchukua nafasi za maafisa wakuu katika jeshi, polisi na idara za usalama.

XS
SM
MD
LG