Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 16:13

Sudan Kusini yaongezewa muda wa vikwazo hadi mwakani


Mabango katika mji mkuu Juba, yakimuonesha Rais Salva Kiir (L) na Makamu Rais wake, Riek Machar.
Mabango katika mji mkuu Juba, yakimuonesha Rais Salva Kiir (L) na Makamu Rais wake, Riek Machar.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja lilipitisha azimio Jumanne kuendeleza tena vikwazo dhidi ya viongozi wa Sudan Kusini kwa mwaka mwingine.

Vikwazo hivyo ni pamoja na marufuku ya kusafiri na kuzuia mali za watu wanaoaminika kuduamaza juhudi za amani na uthabiti nchini humo.

Mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wa kupitisha azimio la kuendeleza vikwazo kwa Sudan Kusini ambao ulidumu kwa takriban dakika 20 tu, lakini upigaji kura una maana kuwa vikwazo vimeongezewa muda mpaka mwisho wa mwezi Mei mwaka 2017.

Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, David Pressman
Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, David Pressman

Akihutubia kwenye baraza la usalama muda mfupi kabla ya upigaji kura, David Pressman, mwakilishi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa katika masuala maalum ya kisiasa alisema muendelezo huo unapeleka ujumbe kwa watunga sera na viongozi wa kisiasa mjini Juba.

Alisema azimio la leo ni vyema liwakumbushe viongozi wa Sudan Kusini kwamba hakuna njia nyingine na hakuna uchaguzi mwingine isipokuwa kutekeleza kwa ukamilifu mkataba wa amani.

Mwishoni mwa mwezi April baada ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini, Riek Machar kurejea Juba, Donaldh Booth, mwakilishi maalum wa Marekani kwa Sudan na Sudan Kusini alitoa ushahidi kwenye bunge la Marekani akisema serikali yake iko tayari kuchukua hatua zozote ikiwa ni pamoja na vikwao na marufuku ya silaha kwa viongozi wa Sudan Kusini.

XS
SM
MD
LG