Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 19:20

Sudan Kusini yadai kuzima jaribio la mapinduzi


Corbit Larson clears snow in front of his Centre Music store in Framingham, Massachusetts. A long duration winter storm that began on Feb. 7 night remains in effect for a large swath of southern New England until the early morning hours on Feb. 10, 2015.
Corbit Larson clears snow in front of his Centre Music store in Framingham, Massachusetts. A long duration winter storm that began on Feb. 7 night remains in effect for a large swath of southern New England until the early morning hours on Feb. 10, 2015.
Hali ingali ya wasiwasi katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, kufuatia usiku wa mapambano katika kile serikali ya nchi hiyo ilichodai ni jaribio la mapinduzi. Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir anasema wanajeshi wanaomtii makamu rais wa zamani walijaribu kufanya mapinduzi lakini walizingirwa na majeshi ya serikali. Rais Kiir ametangaza amri ya kutotoka nje nyakati za usiku katika mji wa Juba.

Katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu Rais Kiir alisema kundi moja la wanajeshi waasi na Makamu Rais wa zamani Riek Machar walifanya shambulizi Jumapili jioni kwenye makao makuu ya jeshi.

Mashahidi waliripoti kusikia milio mizito ya risasi na milipuko katika mji mkuu Jumatatu asubuhi.

Rais Kiir alisema serikali hivi sasa imedhibiti hali hiyo. “Ninapenda kuwaarifu wote, raia wapendwa, kwamba serikali yenu inadhibiti kikamilifu hali ya usalama huko Juba. Washambuliaji walikimbia na majeshi yenu ya usalama yanawasaka. Ninawaahidi leo kwamba sheria itachukua mkondo wake”.

Machar ambaye alitangaza nia yake ya kuwania nafasi ya rais aliondolewa katika wadhifa wake wa makamu rais mwezi Julai kufuatia kuvunjwa kwa baraza la mawaziri na nafasi nyingine.

Akiwa mkosoaji mkuu wa Rais, Machar katika siku za karibuni alimshutumu bwana Kiir kwa kuendesha serikali kama diktekta. Si Machar wala msemaji wake walioweza kupatikana mara moja kuhusiana na matamshi hayo.

Katika kujibu mapigano bwana Kiir ametangaza amri ya kutotoka nje nyakati za usiku mjini Juba kwa muda usiojulikana.

Safari za ndege za kimataifa kwenda na kutoka Juba zimesimamishwa.
Umoja wa Mataifa unasema mamia ya raia wanaomba hifadhi ya ukimbizi katika ofisi zilizopo mjini Juba.
XS
SM
MD
LG