Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 12:40

Upinzani wa Sudan Kusini watupilia mbali matamshi ya maafisa wa Marekani


Mwakilishi maalum wa Marekani nchini Sudan nna Sudan Kusini Donald Booth akizungumza na ujumbe wa Sudan Kusini.
Mwakilishi maalum wa Marekani nchini Sudan nna Sudan Kusini Donald Booth akizungumza na ujumbe wa Sudan Kusini.

Upinzani wa Sudan Kusini umetupilia mbali matamshi ya maafisa wa Marekani ya kumhimiza makamu rais wa zamani wa nchi hiyo Rick Machar kutorudi Sudan Kusini kudai nafasi yake, wakisema kwamba kutokuwepo kwa kiongozi huyo wa upinzani kunazuia hatua hiyo ya amani iliyo na utete.

Balozi Donald Booth mwakilishi maalum wa Marekani Sudan na Sudan Kusini aliwaambia wabunge wa kamati ya mambo ya nje jumatano kwamba Machar ambaye alikimbia nchi mwezi Julai asirudi Sudan Kusini kwasababu ya kuendelea hali ya kutokuwepo uthabiti nchini humo.

Katika mahojiano na Sauti ya Amerika baada ya kikao hicho Booth amesema kutokuwepo kutokuaminiana kati ya Machar na rais wa nchi hiyo Salva Kiir kumepelekea kuwepo na moja ya hali mbaya ya kibinadamu duniani.

XS
SM
MD
LG