Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:47

Sudan Kusini na kaskazini zakaribia muafaka


Rais wa Sudan Omar al Bashir.
Rais wa Sudan Omar al Bashir.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clintion anatarajiwa kuhudhuria kikao cha mwisho cha mkutano huo Jumatatu.

Marais wa Sudan Kusini na Kaskazini wanakaribia kufikia muafaka wa kuondoa majeshi katika eneo wanalozozania la Abyei kabla upande wa Kusini kujitenga rasmi kama taifa huru July 9.

Mwandishi wa VOA Peter Henlein anaripoti kuwa kiongozi wa Sudan Kaskazini Omar al Bashir na yule wa Kusini Salva Kiir walianza mazungumzo Jumapili katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa.

Amesema wamekutana na jopo la juu la maafisa wa Umoja wa Afrika ikiwa ni pamoja na waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi na rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki na kwamba mazungumzo yanategemewa kuendelea Jumatatu.

Taarifa ya Umoja wa Afrika imesema ajenda ya mkutano wa Sudan inahusu pia kuondolewa kwa majeshi yenye silaha katika mkoa wa wenye mzozo wa Abyei pamoja na kupelekwa kwa tume ya kimataifa ya kuhimiza amani itakayoongozwa na Waafrika.

Mjumbe maalum wa Marekani kwa Sudan Princeton Iyman ameiambia Sauti ya Amerika kuwa waziri mkuu wa Ethiopia ambaye ni mwenyeji wa mazungumzo hayo amekuwa na jukumu zito katika juhudi za kupunguza mivutano kati ya kaskazini na Kusini. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton anatazamiwa kuhudhuria kikao cha mwisho cha mkutano huo Jumatatu.

XS
SM
MD
LG