Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 18:54

Wachambuzi wana mashaka kama amani ya Sudan Kusini itadumu


Rais Salva Kiir akipeana mkono na aliyekuwa kiongozi wa uasi, Riek Machar baada ya mazungumo ya Arusha, Tanzania. Jan. 2015.
Rais Salva Kiir akipeana mkono na aliyekuwa kiongozi wa uasi, Riek Machar baada ya mazungumo ya Arusha, Tanzania. Jan. 2015.

Sudan Kusini ambayo ilijipatia uhuru wake mwaka 2011, imesimamisha vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuwajumuisha viongozi wa pande zote mbili katika serikali ya mpito ambado itaiongoza nchi kabla ya uchaguzi kuitishwa katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Rais Salva Kiir, kutoka kabila la Dinka , anafanya kazi pamoja na makamu wa kwanza wa rais Riek Machar ambaye ni wa kabila la Nuer, kama walivyofanya katika kipindi cha miaka miwili ya kwanza baada ya Sudan Kusini kujipatia uhuru. Na kwa sasa, amani ambayo ilimaliza mzozo wa zaidi ya miaka miwili bado ingalipo huku Marekani na wengine wakiangalia hali hiyo kwa umakini mkubwa.

Mfuatiliaji mmoja kuhusu hali ya huko ni mwandishi wa jarida la Foreign Policy, Siobhan O’grady ambaye alimhoji Machar, anasema amani inalegalega.

"Wasi wasi wangu mkubwa hivi sasa ni kitu gani kitatokea . Hali ni tete sana kwa pande zote mbili, na Machar akiwa huko mji mkuu kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenywe mwishoni mwa mwaka 2013, kitu chochote kinaweza kutokea," Anasema O'grady.

Mzozo ulizuka wakati majeshi yanayomtii Kiir yalipopambana na upande wa Machar, na baadaya Machar kushutumiwa kuhusu njama za jaribio la mapinduzi dhidi ya rais.

Mazungumzo ya amani yalianza haraka Addis Ababa Ethiopia, lakini utaratibu ulichukua mpaka Agosti mwaka 2015 kufikia kile kinachoitwa mkataba wa azimio la kumaliza mzozo katika jamhuri ya Sudan Kusini, ambalo lilitaka kuundwa kwa serikali ya mpito inayojumuisha pande zote.

XS
SM
MD
LG