Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:50

Biden:Kura ya maoni muhimu kwa amani Sudan


Makamu rais wa Marekani asema kura ya maoni Sudan Kusini ni muhimu sana kwa amani ya Sudan.

Makamu rais wa Marekani Joe Biden anasema kura ya maoni inayokuja Sudan Kusini ni lazima iwe huru na ya haki kuendeleza uthabiti wa amani mashariki ya Afrika.

Katika mahojiano na shirika la televisheni la ABC, kipindi cha "This Week," Biden alisema kura hiyo ni lazima ionekane kuwa ya uaminifu ili kuifanya Sudan na nchi za jirani ipate maendeleo ya amani. Alisema, "Kitu ambacho hatutaki ni taifa jingine lililoshindwa katika eneo hilo."

Kura ya maoni iliyopangwa kufanyika Januari 9 mwakani itaamua endapo Sudan Kusini inabaki kama sehemu ya Sudan au inakuwa nchi huru. Watu katika jimbo lenye utajiri wa mafuta Abyei watapiga kura siku hiyo hiyo kuamua endapo wataungana na kusini na watabakia kaskazini.

Kura hiyo ya maoni ni sehemu ya makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwaka 2005 kumaliza miaka 21 ya vita baina ya kusini na kaskazini.

XS
SM
MD
LG