Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 19, 2025 Local time: 07:08

Sudan Kaskazini yadhibiti Abyei


Rais wa Sudan Omar al- Bashir
Rais wa Sudan Omar al- Bashir

Wanajeshi wa Sudan Kusini wafukuzwa Abyei

Serikali ya Sudan Kaskazini inasema imedhibiti eneo la Abyei, na kuzusha hofu ya kuzuka kwa mapigano mapya ya wenyewe kwa wenyewe na Sudan Kusini huku eneo hilo likijiandaa kwa uhuru wake.

Amin Hassan Omar, waziri anayehusika na maswala ya rais, aliwaambia mkutano wa waandishi habari Jumapili kuwa vikosi vya Kaskazini mwa Sudan vinaondoa vikosi vyote vya Sudan Kusini katika eneo la Abyei.

Jeshi la Sudan Kaskazini lilipita mji mkuu wa Abyei, huku majeshi yake yakitawanya majeshi ya Sudan Kusini na kusababisha wakazi wengi kutoroka kwa usalama wao.

Khartoum pia imetangaza amri ya kuvunja utawala wa mji wa Abyei.

Ghasia kati ya kaskazini na kusini katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Abyei zimeongezeka katika siku za hivi karibuni, na hali yake ya baadaye bado haijaamuliwa huku upande wa Sudan Kusini ukijiandaa kutangaza rasmi uhuru wake kutoka Kaskazini Julai 9 mwaka huu.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir ameonya kuwa serikali yake haitatambua Sudan Kusini kama taifa huru ikiwa itaendelea kudai eneo la Abyei.

Wajumbe wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamekwenda Khartoum Jumapili kwa mazungumzo juu ya swala la Abyei.

XS
SM
MD
LG