Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 03, 2023 Local time: 20:34

Sudan huenda ikatimbukia kwenye uharibifu, aonya Guterres


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema Jumatatu kwamba Sudan inatumbukia kwenye uharibifu mkubwa na vifo kwa kasi kubwa, wakati akiomba wahisani kuingilia kati ili kuzuia janga hilo.

Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa kutoa ahadi ili kusaidia miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa na mashirika ya wakimbizi, Misri, Ujerumani, Qatar na Saudi Arabia. Ameongeza kusema kwamba bila msaada wa kimataifa, Sudan huenda likawa taifa lisilo fuata tena sheria na kwa hivyo kuchangia ukosefu wa usalama wa kikanda.

Umoja wa Mataifa umetoa ombi mara mbili, moja likiwa msaada wa kibinadamu ndani ya Sudan na la pili ni kusaidia wakimbizi waliotoroka nje ya nchi. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, dola bilioni 3 zinahitajika mwaka huu, lakini ni asilimia 17 pekee zilizotolewa.

Guterres ameongeza kusema kwamba fedha zilimiminika kwenye Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Ukraine ndani ya wiki kadhaa baada ya uvamizi wa Russia Februari mwaka jana, lakini hali imekuwa tofauti kwa Sudan, sasa hivi mapigano yakiwa yamepita miezi miwili.

Ameongeza kusema kwamba njia pekee ya kumaliza mgogoro uliopo ni kupitia kurejesha amani pamoja na utawala wa kiraia kwa kutumia mpito wa kidemokrasia. Umoja wa Afrika pamoja na Umoja wa Ulaya pia wapo kwenye mtari wa mbele kwenye juhudi hizo.

Forum

XS
SM
MD
LG