Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 07:09

Sudan Kusini yaishutumu Kaskazini kwa njama


Raia mmoja wa Sudan akionyesha uungaji mkono kwa kura ya maoni kwa ajili ya uhuru wa Sudan kusini, ilikuwa wakati wa mkutano ulioandaliwa na baraza la kura ya maoni kwa Sudan Kusini huko Juba, mwezi January kabla ya upigaji kura.
Raia mmoja wa Sudan akionyesha uungaji mkono kwa kura ya maoni kwa ajili ya uhuru wa Sudan kusini, ilikuwa wakati wa mkutano ulioandaliwa na baraza la kura ya maoni kwa Sudan Kusini huko Juba, mwezi January kabla ya upigaji kura.

Sudan Kusini imesitisha mazungumzo ya kujitenga na kasakzini, ikiishutumu Khartoum kwa kupanga kuiangusha serikali ya kusini na kuua watu wake.

Pagan Amum, afisa mwandamizi katika chama tawala cha kusini, amesema jana jumamosi kwamba kaskazini inawapatia mafunzo na silaha wanamgambo ili kuidumaza Sudan Kusini na kuwang'oa viongozi wa eneo hilo kabla ya ya kujitenga mwezi July.

Amum alizungumza tena hivi leo, nakusema chama tawala huko kaskazini kinayapatia makabila ya kiarabu silaha ili kwa maneno yake, wafanya mauaji ya halaiki kama yale yaliyofanywa huko Darfur.

Hakuna ripoti majibu ya haraka kutoka chama tawala cha National Congress huko kaskazini kwa matamshi ya karibuni ya Amum. Jana jumamosi, maafisa wa NCP walipuuza shutuma za Amum wakisema hazina msingi.

Sudan Kusini imekumbwa na wimbi la mapambano ya kutisha na makundi ya waasi katika miezi ya karibuni. Jeshi la kusini linasema waasi 23 waliuawa jumamosi baada ya kushambulia Malakal, mji mkuu wa jimbo lenye utajiri wa mafuta la Upper Nile huko kusini.

Wakusini kwa idadi kubwa walipiga kura kudai uhuru kutoka kaskazini mwezi January.

Upiaji kura uliahidiwa katika mkataba wa amani wa mwaka 2005 ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe kati kusini na kaskazini ambavyo vilidumu kwa takriban miaka 21.

Mapigano yanaendelea katika mkoa wa magharibi wa Darfur huko nchini Sudan, ambako waasi wameshika silaha dhidi ya serikali tangu mwaka 2003. Mahakama ya kimataifa ya uhalifu imemshtaki rais Omar Al Bashir kwa tuhuma za uhalifu wa vita na mauaji ya halaiki katika mkoa huo.

Sudan Kusini inatarajiwa kujitenga na kaskazini hapo July 9. Hatahivyo pande zote bado hazijasuluhisha masuala kadhaa makuu, ikiwemo hali ya mkoa wenye utajiri wa mafuta wa Abyei, ambapo uko kwenye mpaka kati ya kusini na kaskazini.

XS
SM
MD
LG