Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 10:53

Trump bado anaamini wizi mkubwa wa kura ulimzuia kupata kura ya umaarufu


Msemaji wa White House, Sean Spicer

Ikulu ya White House imesema Jumanne kuwa Rais Donald Trump bado anaamini kuwa milioni ya kura zilizopigwa na wahamiaji wasio halali zilisababisha kukosa kura za umaarufu katika uchaguzi wa Novemba.

“Ni imani anayoendele kuwa nayo,” msemaji wa ikulu ya White House, Sean Spicer amewaambia waandishi, siku moja baada ya rais mpya kurejea kauli yake katika tafrija ya viongozi wa bunge, madai yasiyo na ushahidi kwamba wahamiaji milioni 3 mpaka 5 nchini walipiga kura batili kumpa mpinzani wake, mdemokrat Hillary Clinton

Spicer hakutoa ushahidi wowote kuhusu wizi huo wa kura. Akishinikizwa na waandishi kuonyesha ushahidi aliokuwa nao Trump, Spicer amesema Trump “ anaendelea kuamini hilo kwa sasa, kwa kuegemea tafiti na taarifa alizokuwa nazo.”

Maafisa wa uchaguzi

Lakini maafisa wa uchaguzi ambao wamefanya uchambuzi juu ya kura za Novemba 8 wamesema kwa sehemu kubwa kulikuwa hakuna dalili ya wizi wa kura—na bila shaka sio katika kiwango wa kile anachosema Trump.

Waandishi wengi waliokuwaJumanne kwenye mkutano wa waandishi White House walimuuliza Spicer, ni kwa nini rais kama anaamini kulikuwa na wizi wa kura uongozi wake usianzishe uchunguzi.

Spicer amesema Trump ana uhakika wa ushindi wake wa kura za wajumbe (Electoral College) na anataka kufuatilia utelekelezaji wa ahadi za kampeni kwa wamarekani waliomchagua. Lakini aliposhinikizwa tena kuhusu madai ya wizi wa kura na waandishi, Spicer amesema uchunguzi bado unaweza kufanyika siku za usoni.

Majibu ya Warepublikani

Lakini kiongozi wa warepublikani katika bunge spika Paul Ryan amewaambia waandishi yeye hajaona ushahidi wowote wa wizi wa kura mkubwa katika uchaguzi wa 2016.

Kiongozi wa walio wengi katika baraza la Seneti, mrepublikan Mitch McConnell amewaambia waandishi kuwa wizi wa kura unatokea akiongeza: “ Siku zote kuna malumbano pande zote mbili juu ya ukubwa wa wizi huo, na kwa wingi gani na yote mengineyo.”

Seneta Graham

Seneta wa South Carolina Lindsey Graham, mmoja wa waliokuwa katika kinyang’anyiro cha urais ambaye Trump alimshinda katika mbio za uchaguzi mkuu dhidi ya Clinton, amemuasa rais kuacha kurejea madai yake hayo na kusema kama ana ushahidi wa wizi, “ni lazima aelezee kwa nini anaamini hilo.”

Clinton alishinda kura za umaarufu dhidi ya Trump kwa takriban kura milioni 3. Lakini Trump alishinda pale penye kumpa ushindi—nako ni kwenye kura za wajumbe. Mfumo wa uchaguzi wa Marekani unawachagua marais, kupitia matokeo ya uchaguzi wa jimbo kwa jimbo ambao unampata mshindi, na sio jumla ya kura zote nchini.

Graham ambaye alijitoa katika kinyang’anyiro hicho kwa kumwachia mteule wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Republikan baada ya kupata kura chache sana, amesema, “Nitapenda rais aachane na jambo hili kabisa. Hii ni demokrasia kubwa kuliko zote ulimwenguni; sisi ni viongozi wa dunia huru, na watu wataanza kututilia mashaka kama mmoja wetu ikiwa ataendelea kutoa tuhuma dhidi ya mfumo wa uchaguzi wetu bila ya kutoa ushahidi. Hili litadhoofisha uwezo wake wa kuongoza nchi hii kama hajaacha malalamiko haya.”

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG