Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 11:22

Uruguay vs Ureno, Russia vs Spain katika raundi ya pili


Cristiano Ronaldo katika mechi na Iran 25 Juni 2018.
Cristiano Ronaldo katika mechi na Iran 25 Juni 2018.

Uruguay imekuwa timu ya kwanza katika fainali za kombe la dunia 2018 kumaliza awamu ya makundi kwa kushinda mechi zake zote tatu na kutoka na pointi tisa juu ya Kundi A baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji Russia Jumatatu, siku ambayo timu za Kundi A na B zilicheza mechi zao za mwisho katika awamu hiyo. Uruguay sasa itapambana na Ureno Jumamosi.

Russia nayo imefanikiwa kuingia katika raundi ya 16 ambapo itapambana na Spain Jumapili baada ya kushika nafasi ya pili kwenye kundi lake ikiwa na pointi sita kwa kushinda mechi zake mbili za kwanza dhidi ya Misri na Saudi Arabia.

Spain na Ureno zimeingia raundi ya 16 baada ya kutoa sare na wapinzani wao na hivyo kumaliza na pointi tano kila moja. Spain ilitoka sare 2-2 na Morocco wakati Ureno ilitoka sare 1-1 na Iran. Spain ilikuwa katika hali ngumu hadi goli lake la kusawazisha katika dakika za nyongeza ambalo lilikubaliwa baada ya muamuzi kwenda katika video.

Spain yapata goli la kusawazisha dakika za nyongeza
Spain yapata goli la kusawazisha dakika za nyongeza

Kutoka kundi A, Misri na Saudi Arabia zinarudi nyumbani ingawa Saudi Arabia imemaliza na pointi tatu baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Misri katika mechi yao mwisho. Misri imetoka patupu lakini nyote wake Mohammed Salah angalau ana rekodi ya magoli mawili ya kombe la dunia katika historia yake.

Kutoka kundi B Iran na Morocco zimeaga mashindano ingawa Iran ilijipatia pointi 4 na kushika nafasi ya tatu. Morocco ilimaliza mwisho katika kundi hilo ikiwa na pointi moja.

Makundi ya C na D yanacheza mechi zao za mwisho Jumanne huku macho ya Waafrika yakiwa katika kile kinachoitwa ‘fainali’ ya Kundi D baina ya Nigeria na Argentina. Timu hizo zinawania kujiunga na Croatia kutoka kundi hilo kwenda raundi ya pili. Nigeria ina pointi tatu inahitaji sare na kuomba Croatia iishinde au itoke sare na Iceland – ili kuingia raundi ya pili. Lakini ushindi dhidi ya Argentina utaihakikishia Nigeria raundi ya pili.

Argentina inahitaji ushindi kamili dhidi ya Nigeria ili imalize na pointi nne na wakati huo huo kuomba Croatia iifunge au itokea angalia sare na Iceland.

Katika mechi za kundi C Ufaransa yenye pointi sita inakutana na Denmark yenye pointi nne. Timu hizo zinahitaji kutoka sare tu zote ziingie raundi ya pili. Australia ambayo ina pointi moja inakutana na Peru inayoshika mkia katika kundi hilo bila pointi.

XS
SM
MD
LG