Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 02:30

Sudan Kusini yakaribishwa katika jumuiya ya Afrika Mashariki EAC


Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini.
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini.

Sudan kusini inatazamia kuwa na uhusiano thabiti na majirani zake kadhalika na soko kubwa ambalo litakuwa wazi kufanya biashara baina ya mataifa ya EAC, na kunufaisha raia wote katika kanda hio.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir anafurahia uwezekano wa matarajio ya kijamii na kiuchumi baina ya pande mbili, baada ya taifa lake ambalo ni jipya zaidi duniani, kuwa mwanachama rasmi wa jumuiya ya Afika Mashariki Jumatano.

Sudan Kusini ilipigiwa kura kujiunga na taasisi hiyo ya kiuchumi wakati wa mkutano wa viongozi wa kikanda uliofanyika Arusha,Tanzania.

Msemaji wa rais wa Sudan kusini Ateny Wek Ateny, anasema rais Kiir anafuraha kwa Sudan Kusini hatimae kuingizwa katika jumuiya ya Afrika Mashariki. Hakuna masharti ya shughuli au huduma baina ya wanachama wa jumuiya hio na sudan kusini. Kwa hiyo ni vizuri kuwa Sudan Kusini hatimae sasa ni mwanachama.

Bw Ateny anasema, Sudan kusini inatazamia kuwa na uhusiano thabiti na majirani zake kadhalika na soko kubwa ambalo litakuwa wazi kufanya biashara baina ya mataifa hayo, ambayo anasema itanufaisha raia wote katika kanda hio. Anasema kuwa mwanchama wa 6 wa jumuiya hio ni mafanikio makubwa kwa serikali ya juba.

Wanachama wengineo ni pamoja na Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.

Baadhi ya raia wa Sudan Kusini wanasema bado wanasubiri kuona jinsi serikali ya muungano ya mpito itashughulikia hadhi mpya ya taifa hilo kama mwanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki. Rais Kiir anatarajiwa kuunda serikali pamoja na mpinzani wake Riek Machar, kufwatia makubaliano ya kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

XS
SM
MD
LG