Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 10:18

Sudan Kusini kuwekewa vikwazo vya silaha


Riek Machar alietoroka Sudan Kusini baada ya mapigano kuzuka.
Riek Machar alietoroka Sudan Kusini baada ya mapigano kuzuka.

Umoja wa Mataifa pamoja na wanachama 15 wa baraza la usalama la Umoja huo Alhamisi walipitisha rasimu ya azimio la kuweka marufuku ya silaha kwa Sudan Kusini.

Umoja wa Mataifa pamoja na wanachama 15 wa baraza la usalama la Umoja huo Alhamisi walipitisha rasimu ya azimio la kuweka marufuku ya silaha kwa Sudan Kusini iliyolenga zaidi vikwazo kufuatia onyo lililotolewa na afisa mwandamizi wa Umoja huo la uwezekano wa kutokea kwa mauaji ya halaiki.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters,uhasimu wa kisiasa kati ta Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir kutoka kabila la Dinka na makamu wake wa zamani Riek Machar kutoka kabila la Nuer ulipelekea kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 ambavyo vinaaminika kuchochewa na misimamo ya kikabila.

Viongozi hao walitia saini mkataba wa Amani mwaka jana, lakini licha ya hatua hiyo, mizozo ya kisiasa imeendelea kushuhudiwa na kusababisha Machar kutoroka nchini mwezi Julai.

XS
SM
MD
LG