Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:20

Somaliland yatangaza baraza la mawaziri


Rais mpya wa Somaliland ameteuwa mawaziri 26 na manaibu kuunda baraza lake jipya la mawaziri.

Rais mpya wa Somaliland ameteuwa mawaziri na manaibu 26 kuunda kile alichoita baraza dogo la mawaziri kuliko yote katika historia ya nchi hiyo iliyojitenga kutoka Somalia.

Katika hotuba yake Jumatano Rais Ahmed Mohamed Silanyo alisema hazina ya nchi hiyo haina kitu na serikali yake itafanya kazi ya ziada kuboresha uchumi wa nchi. Alisema pia kuwa atashirikiana kikamilifu na jumuiya ya kimataifa.

Rais Silanyo alimshinda kiongozi aliyekuwa madarakani Dahir Riyale Kahin katika uchaguzi wa Juni. Somaliland ilijitangazia uhuru wake kutoka Somalia mwaka 1991.

Huko Somalia kwenyewe maafisa wamesema Jumatano watu wasiopungua 11 wameuawa katika mapigano mapya baina ya waasi wa kiislamu na majeshi ya serikali. Mapigano yalizuka Jumanne jioni waasi wa kundi la Hizbu Islam waliposhambulia maeneo yanayoshikiliwa na serikali.

XS
SM
MD
LG