Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 14:55

Mahiga: Lazima kuziba pengo lililoachwa na al-Shabab


Vikosi vya Somalia msituni vikijiandaa kupambana na kundi la kigaidi la al-Shabaab katika kitongoji cha soko la Bakara, Mogadishu, Mei 22, 2011.
Vikosi vya Somalia msituni vikijiandaa kupambana na kundi la kigaidi la al-Shabaab katika kitongoji cha soko la Bakara, Mogadishu, Mei 22, 2011.

Balozi Augustine Mahiga asema kundi al-Shabaab limeondoka Somalia

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia Balozi Augustine Mahiga, anasema kundi la wanamgambo wa al-Shabaab lenye ushirika na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida limeondoka Somalia, lakini anatahadharisha kuwa huenda kukaibuka makundi ya kujazia pengo lililoachwa na al-Shabaab.

Mahojiano na Balozi Mahiga

Akizungumza na Sauti ya Amerika Alhamis, akiwa mjini Kampala ambapo alitazamiwa kukutana na Rais Yoweri Museveni, Balozi Mahiga alisema ameliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika kuongeza juhudi na mchango wao wa kijeshi kusaidia serikali ya Somalia ili iweze kujenga mfumo thabiti wa utawala na taasisi za kutegemewa kwa raia wa Somalia.

Aidha Balozi Mahiga, alisema mkusanyiko wa maswala kadha huenda ulipelekea kuvunjwa nguvu kwa kundi hilo la al-Shabaab, ikiwemo ukosefu wa fedha, kukosa uongozi thabiti na hata matatizo ya njaa na ukame.

Lakini alisitiza kuwa kulikuwa na mapambano makali baina ya al-Shabaab na vikosi vya serikali ya Somalia vikisaidiwa na majeshi ya Umoja wa Afrika-AMISOM kwa siku 10 hivi, kabla ya kundi hilo kusalim amri.

Kuhusu ukame na njaa iliyokumba Somalia, Balozi Mahiga alisema alianza kuonya juu ya uwezekano wa kuibuka janga kubwa la njaa tangu mwezi Oktoba mwaka jana, kwa kutoa taarifa kwa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Anasema endapo jamii ya kimataifa ingeliingilia kati tangu wakati huo, maafa na picha za kuhuzunisha zinazoshuhudiwa na dunia nzima kuhusu njaa nchini Somalia yangeepukika.

Mjumbe huyo maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia pia, alisema yupo tayari kuhamia Mogadishu, na anahimiza jamii ya kimataifa ichangie kuhamishia makao ya ofisi yake mjini humo badala ya Nairobi ili kuweza kutoa huduma zaidi na kwa wakati ufaao, kusaidia kuleta uthabiti wa kiutawala nchini Somalia.

XS
SM
MD
LG