Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 08:13

Somalia yaomba marufuku ya silaha iondolewe


Kundi la wanamgambo wa Alshabab Somalia.
Kundi la wanamgambo wa Alshabab Somalia.

Taarifa ya serikali ya Somalia yasema muungano wa Alshabab na Alqaida waongeza wasi wasi wa usalama nchini Somalia.

Serikali ya Somalia imetoa wito wa kumalizika kwa marufuku ya silaha nchini humo, ili iweze kupambana vizuri zaidi na kundi la wanamgambo wa kiislam la Alshabab. Taarifa ya serikali Jumatatu imesema muungano wa Alshabab na al qaida uliotangazwa wiki iliyopita utaongeza wasi wasi juu ya hali ya kiusalama nchini Somalia. Imesema Somalia inaweza kuwa ngome ya mtandao wa kigaidi. Serikali imesema ingependa kuona kuondolewa kwa marufuku ya kuingiza silaha nchini humo iliyowekwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1992 baada ya serikali ya mwisho ya Somalia iliyogubikwa na utata kuanguka na nchi kutumbukia kwenye ghasia.

XS
SM
MD
LG