Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:48

Somalia yachagua rais mpya


Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, aliyechaguliwa Sept. 10, 2012
Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, aliyechaguliwa Sept. 10, 2012
Rais mpya wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamed ameapishwa rasmi kuchukuwa madaraka baada ya kumshinda rais anaeondoka madarakani Sharif Sheikh Ahmed. Kiongozi mpya aliapishwa mbele ya wabunge na wageni wa heshima na Mwanasheria Mkuu Abdullahi Ilka-hanaf, Jumatatu usiku.

Mohamud alijipatia kura 190 dhidi ya mpinzani wake Shiekh Ahmed aliyepata kura 79 katika duru ya tatu na mwisho ambayo wabunge 269 walishiriki.Kulikuwepo na wagombea 22 walopigania kiti cha rais katika duru ya kwanza na 18 kati yao walioondolewa katika duru hiyo.

Rais mpya, mwenye kiti wa chama kipya cha Amani na Maendeleo PDP alimshukuru rais wa zamani kwa kazi yake kwa kile alichokieleza ni "utaratibu wa kihistoria." Alimshukuru kwa kuwezesha mabadiliko haya yaliyopelekea uchaguzi wa kihistoria wa hii leo.

Ni uchaguzi wa kwanza wa rais kufanyika Somalia katika kipindi cha zaidi ya miaka 20. na rais mpya alishukuru Jumuia ya Kimataifa kwa kuwasaidia Wasomalia wakati wa utaratibu huu..

Akizungumza baada ya kula kiapu Bw Mohamud alisema anahirtaji msaada wa Wasomali wote katika kugeuza ukurasa huu mpya kwa ajili ya Somalia.

"Ninataka kuwaomba Wananchi wa Somalia kumunga mkono, kwa kila njia, ili kubuni serikali yenye nguvu itajkayofanya kazi kote Somalia."

Rais anaeacha madaraka Sharif Sheukh Ahmed alisema anakubali matokeo ya uchaguzi na kumpiongeza ndugu yake Mohamud kama rais mpya , na kusema anakubaliana na matokeo yaliyokuwa ya haki .
XS
SM
MD
LG