Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 11:21

Mapigano yaongezeka Somalia

Mabaki ya damu katika hoteli ya Muna, mjini Mogadishu iliyoshambuliwa na kundi la al-Shabab 24 Aug 2010
Mabaki ya damu katika hoteli ya Muna, mjini Mogadishu iliyoshambuliwa na kundi la al-Shabab 24 Aug 2010

Mapigano zaidi yamezuka katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, siku moja baada ya wanamgambo wa al-Shabab kuvamia hoteli moja na kuuwa zaidi ya watu 30.

Mapigano zaidi yamezuka katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, siku moja baada ya wanamgambo wa al-Shabab kuvamia hoteli moja na kuuwa zaidi ya watu 30.

Mashahidi wanasema al-Shabab na majeshi yanayounga mkono serikali yalifyatuliana silaha kali Jumatano. Watu wasiopungua sita waliripotiwa kufa. Makamanda kutoka upande wa serikali walisema walishikilia nafasi zao kukabiliana na mashambulizi ya usiku kucha yaliyofanywa na al-Shabab.

Jumanne, wanamgambo wa al-Shabab walivamia hoteli moja katika moja ya maeneo machache ya Mogadishu yanayodhibitiwa na serikali. Katika taarifa ya Jumatano, Wizara ya Habari ya Somalia imeongeza idadi ya vifo kutokana na shambulizi hilo kufikia 33, wakiwemo wabunge wanne.

Marekani imelaani vikali shambulizi hilo. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje P.J Crowley alisema ikizingatiwa kwamba shambulizi lilitokea wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan inaonyesha jinsi al-Shabab linavyopuuza mwezi huu kwa kutokuthamini maisha ya watu, mila ya kisomali na uislam.

XS
SM
MD
LG