Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:29

Maharamia Somalia wameiachia meli.


Boti ya maharamia wa Somalia.
Boti ya maharamia wa Somalia.

Maafisa wa safari za baharini wanasema maharania wa Somalia wameachia meli ya mizigo ambayo ilikuwa imetekwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

Maafisa wa safari za baharini wanasema maharania wa Somalia wameachia meli ya mizigo ambayo ilikuwa imetekwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

Meli hiyo - Talca - na wafanyakazi wake 23 raia wa Sri Lanka, raia mmoja wa Filipino na raia mmoja wa Syria waliachiwa Jumanne asubuhi. Maafisa hao wanasema maharamia walilipwa fidia ingawa haijulikani ni kasi gani.

Maafisa wanasema wafanyakazi wote wako salama.
Meli hiyo ilitekwa nyara kwenye ufukwe wa Oman Machi 23.
Wakati huo huo afisa wa cheo cha juu katika wizara ya ulinzi ya Russia anasema maharamia 10 waliokamatwa na majeshi yake na kisha kuachiwa huru wiki iliyopita huwenda wamekufa kwenye bahari.

Afisa huyo aliwaambia waandishi wa habari Jumanne maharamia hao waliachwa baharini bila ya kupatiwa chombo cha kuwasaidia kusafiria. Wanajeshi maalumu wa Russia waliwakamata maharamia hao baada ya kuteka nyara meli moja ya mafuta ya Russia iitwayo Moscow University, katika mwambao wa Pembe za Afrika.


XS
SM
MD
LG