Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:30

Somalia kufanya uchaguzi wa rais May 15


Waziri mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble -katikati- ahudhuria sherehe za kuapishwa kwa wabunge wepya mjini Mogadishu, April 14, 2022. Picha ya Reuters
Waziri mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble -katikati- ahudhuria sherehe za kuapishwa kwa wabunge wepya mjini Mogadishu, April 14, 2022. Picha ya Reuters

Somalia itafanya uchaguzi wa rais tarehe 15 mwezi huu, kituo cha televisheni cha taifa kimetangaza Alhamisi, kikinukuu taarifa ya kamati ya bunge iliyopewa jukumu la kuandaa uchaguzi ambao ulicheleweshwa kwa muda mrefu katika taifa hilo lenye uthabiti dhaifu la Pembe ya Afrika.

Uchaguzi huo utafanyika baada ya mwaka mmoja kuliko ilivyokuwa imepangwa na ratiba, baada ya mchakato wa maandalizi ya uchaguzi kukumbwa na ghasia mbaya pamoja na mvutano wa kuwania madaraka kati Rais Mohamed Abdullahi Mohamed, maarufu Farmajo, na Waziri mkuu Mohamed Hussein Roble.

Washirika wa kimataifa wa Somalia wamekuwa wakishinikiza ili mchakato huo uongeze kasi, wakihofia kwamba kucheleweshwa kwa uchaguzi kutadhoofisha juhudi za kukabiliana na matatizo mengi yanayolikumba taifa hilo, ikiwa ni pamoja na vita dhidi ya wanajihadi wa Al Shabaab na tishio la njaa.

“Kwa kuzingatia hali ya sasa ya nchi, wajumbe wamekubaliana kwamba tarehe 15 Mei itakuwa siku ya uchaguzi wa rais,” Mohamed Ibrahim Moalimu, mjumbe wa kamati ya uchaguzi ya bunge, amesema Alhamisi katika ujumbe kwenye ukurasa wa Facebook.

Muda wa msaada wa miaka mitatu wa dola milioni 400 uliotolewa na shirika la kimataifa la fedha (IMF) utamalizika moja kwa moja katikati ya mwezi Mei, ikiwa utawala mpya hautakuwepo kufikia wakati huo, hatua ambayo huenda ikaitumbukiza nchi hiyo katika hatari zaidi.

​
XS
SM
MD
LG