Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 23:52

Somalia yatoa sababu ya marufuku ya ndege za miraa kutoka Kenya.


Rais wa Somalia, Sheikh Sheriff Sheikh Ahmed kushoto akiwa na Waziri Mkuu wake Mohamed Abdullahi Mohamed mjini Mogadishu.
Rais wa Somalia, Sheikh Sheriff Sheikh Ahmed kushoto akiwa na Waziri Mkuu wake Mohamed Abdullahi Mohamed mjini Mogadishu.

Serikali ya Somalia imesema kuwa sababu kuu ya kupiga marufuku ndege za kubeba miraa kutoka Kenya ni kutokana na kukasirishwa na ziara iliyofanywa na Gavana wa Meru Peter Munya katika jimbo lililojitangazia uhuru wake la Somaliland ambalo halitambuliwi kimataifa .

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya, balozi wa Somalia nchini kenya Gamal Hassan, amesema Jumanne jioni kwamba ziara ya Gavana Munya huko Somalilanda imezusha shinikizo la kisiasa lisilohitajika kwa serikali ya Mogadishu na ni kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake.

Gazeti hilo limesema kuwa Gavana Munya, ambaye anatoka eneo linalokuzwa miraa kwa wingi, alizuru Somaliland mnamo mwezi Julai na kufanya mazungumzo na naibu wa rais wa Somaliland, Abdurahman Ishmaiel, pamoja na mawaziri wa mambo ya nje na wa fedha, ambapo yamkini alitaka kanuni zinazohusu usafirishaji wa zao hilo kutoka Kenya zilegezwe, na kuahidi kuwa Kenya ingetambua Somalilanda kama taifa huru.

XS
SM
MD
LG