Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 00:38

Somalia inatishia kusimamisha safari zote za ndege za Ethiopian Airlines


Nembo ya ndege ya shirika la Ethiopia Airlines
Nembo ya ndege ya shirika la Ethiopia Airlines

Mamlaka ya usafiri wa anga ya Somalia imetishia kusimamisha safari zote za ndege za shirika la ndege la Ethiopia kuelekea nchini humo, vyombo vya habari vya serikali vilisema Jumatano, kitendo cha hivi karibuni katika mzozo wa muda mrefu unaohusu jimbo la Somaliland lililojitenga.

Addis Ababa ilisaini mapema mwaka huu mkataba wa maelewano na Somaliland kukodisha kilomita 20 za pwani katika kipindi cha miaka 50, kuiruhusu Ethiopia isiyo na bahari kufika kwenye pwani.

Kwa upande wake, Somaliland ambayo ilitangaza uhuru wake kwa kujitenga na Somalia mwaka 1991, imesema Ethiopia itakuwa nchi ya kwanza kuitambua rasmi Somaliland kama taifa, hatua ambayo haijathibitishwa na Addis Ababa.

Ndege za Ethiopian Airlines zinasafiri hadi mji mkubwa wa Somaliland wa Hargeisa, na mji mkuu wa Somalia Mogadishu na miji minne ya majimbo ya Somalia.

Mamlaka ya anga ya Somalia (SCAA) imesema Ethiopian Airlines inayomilikiwa na serikali, shirika kubwa la ndege barani Afrika, halijashughulikia malalamiko ya hapo awali kuhusu “masuala ya uhuru” na limeondoa taarifa za safari kuelekea Somalia, na kubakiza tu namba za viwanja vya ndege”.

“Hatua hii inazidisha wasiwasi wa awali na kudhoofisha uhuru wa Somalia,” SCAA ilisema katika barua iliyochapishwa na vyombo vya habari vya serikali.

Ikiwa masuala haya hayatakuwa yametatuliwa ifikapo Agosti 23, SCAA haitakuwa na budi ila kusimamisha safari zote za ndege za Ethiopia Airlines kuelekea Somalia, kuanzia tarehe hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG