Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:12

Serikali ya Somalia yamnyonga mwandishi wa zamani kwa kuisaidia Al Shabab kuua


Hassan Hanafi Haji mwandishi wa habari wa zamani akiwa amefungwa kwenye nguzo tayari kwa kunyongwa Mogadishu, Somalia.
Hassan Hanafi Haji mwandishi wa habari wa zamani akiwa amefungwa kwenye nguzo tayari kwa kunyongwa Mogadishu, Somalia.

Serikali ya Somalia imemnyonga mwandishi wa habari wa zamani aliyeshutumiwa kulisaidia kundi la wanamgambo la Al Shabaab kuuwa waandishi wa habari wasiopungua watano mjini Mogadishu kati ya mwaka 2007 na 2011.

Maafisa na mashuhuda wanasema kundi maalumu lilimnyonga Hassan Hanafi Haji leo Jumatatu kwenye chuo cha mafunzo ya polisi mjini Mogadishu. Haji alirejeshwa kutoka Kenya mwaka jana kufuatia ombi la serikali ya Somalia.

XS
SM
MD
LG