Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 08:47

Somalia yaishtaki Kenya kwa kuchukua eneo la mpaka wake


Ramani ikionesha Somalia inavyopakana na nchi ya Kenya.
Ramani ikionesha Somalia inavyopakana na nchi ya Kenya.

Mahakama ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa inasema itasikiliza mzozo wa mpaka wa baharini kati ya Somalia na Kenya baadaye mwaka huu.

Somalia imelalamika kwamba Kenya kwa makosa imedai sehemu za maji yake kwenye bahari ya Hindi maeneo ambayo yana utajiri wa gesi na mafuta.

Mzozo huu unahusu eneo la zaidi ya kilometa za mraba 100,000.

Kenya inaliona eneo lake la mpaka likiwa kwenye mstari ulionyooka kutoka kwenye eneo lake la nchi kavu hadi kwenye bahari ya hindi ambalo litawapa eneo la ziada.

Somalia inasema mstari wa mpaka ni vyema uwe kwenye eneo la nchi kavu katika mwelekeo wa kusini mashariki ambao utalifanya eneo la ziada kuwa ni lao.

XS
SM
MD
LG