Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 13:21

Mchakato wa kupata wabunge Somalia watiwa kasoro


Wananchi wa Somalia wakisoma magazeti katika mitaa ya Mogadishu, May 2011.

Somalia haijaweza kuitisha uchaguzi wa nchi nzima kwasababu ya masuala ya usalama na tatizo la gharama za kuendesha mchakato huo.

Wanachama wa mabaraza mawili ya bunge Somalia wameapishwa baada ya uchaguzi ingawaje kuna malalamiko kuwa mchakato uligubikwa na kasoro na madai ya rushwa.

Hata hivyo kasoro hizi zimeendelea kuchelewesha uchaguzi wa rais wa nchi hiyo kwa mara ya nne sasa.

Sherehe hizo za kuwaapisha wawakilishi hao 281 wa mabaraza yote mawili zilifanyika Jumanne wakati wanakabidhiwa ofisi.

Waandishi wa Sauti ya VOA mjini humo wameripoti kuwa serikali iliongeza ulinzi mitaani wakati wa sherehe hizo.

Mchambuzi wa kanda hiyo, Abdiwahab Sheikh Abdisamad amesema kuapishwa kwao kunaashiria mwanzo wa enzi mpya.

“Wawakilishi hao, takriban asilimia 45 kati yao ni wawakilishi waliokuwepo awali, na asilimia 55 ni vijana wapya, walio na nguvu na ni wasomi wazuri,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa kwa mara ya kwanza, “idadi kubwa” kati yao ni wanawake.

Mohammed Osman Jawari, spika wa bunge linalo maliza muda wake, alitangaza rasmi kukabidhi madaraka kwa kundi la pili la wabunge katika kipindi cha miaka 25.

Wawakilishi hao waliochaguliwa “wameapishwa na kuanzia hivi sasa watakuwa ndio wenye kuhusika na utungaji sheria za nchi,” alisema.

Masuala ya kiusalama, gharama

Somalia haikuweza kufanya uchaguzi nchi nzima kwa sababu ya masuala ya usalama na tatizo la gharama za kuendesha mchakato huo.

Badala yake, wawakilishi wa mabaraza yote walichaguliwa na “wajumbe maalum” takriban na watu 14,000 na ambao baadae walichaguliwa na viongozi wa makabila na wakilishi wa mikoa. Hivi sasa rais atachaguliwa na bunge.

Uchaguzi huo ulikuwa umepangwa kufanyika siku ya Jumatano, lakini maafisa wa Tume ya Uchaguzi wameiambia VOA kwamba uchaguzi huo umeahirishwa hadi Januari 24. Tume bado haijatangaza tarehe hii kwa umma.

Lakini wapinzani wanasema mchakato wa kuwatafuta wabunge ulikuwa umefunikwa na ununuzi wa kura, fujo na vitisho.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG