Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 10:45

Meli ya Urusi yaokolewa


Kikosi maalum cha Russia kimeiokoa meli ya mafuta iliyokuwa na wafanyakazi 23 ambayo ilitekwa nyara na maharamia wa Somalia.

Kikosi maalum cha Russia kimeiokoa meli ya mafuta iliyokuwa na wafanyakazi 23 ambayo ilitekwa nyara na maharamia wa Somalia.

Wanajeshi Marines wa Russia kutoka kwenye meli ya kivita walivamia meli hiyo ya mafuta Moscow University katika shambulizi la alfajiri kwenye Pembe ya Afrika.

Shirika la habari la Russia limesema haramia mmoja aliuwawa na wengine 10 kukamatwa. Nahodha wa meli hiyo anasema wafanyakazi wote wako hai na salama salimini.

Maharamia waliteka meli hiyo iliyokuwa na tani 86,000 za mafuta Jumatano. Wafanyakazi wa meli hiyo wa Russia walijificha kwenye chumba cha usalama ndani ya meli hiyo.
Kampuni ya Novoship inasema uamuzi wa kuvamia meli hiyo ulichukuliwa baada ya kujua wafanyakazi wa meli hiyo wako salama.

XS
SM
MD
LG