Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 10, 2024 Local time: 19:19

Siku ya Ukimwi Duniani : Wagonjwa wa Ukimwi wana fursa nyingi zaidi za matibabu


Ribon nyekundu ikiwa ni kumbukumbu ya Siku ya Ukimwi Duniani White House. REUTERS/Jonathan Ernst
Ribon nyekundu ikiwa ni kumbukumbu ya Siku ya Ukimwi Duniani White House. REUTERS/Jonathan Ernst

Disemba 1, wengi huadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani kuonyesha uungaji mkono wale wanaoishi na virusi vya HIV na kuwaenzi wale waliokufa kutokana na maradhi yanayohusiana na Ukimwi.

Matibabu yamepitia njia ndefu kwa wale walioathirika na HIV, lakini tiba bado haijajulikana.

Ulimwenguni, kiasi cha watu milioni 38 wanaishi na HIV. Tangu virusi hivyo vilipogunduliwa mwaka 1984, zaidi ya watu milioni 36 wamefariki kutokana na HIV – au magonjwa yanayohusiana na Ukimwi.

Kila mwaka ifikapo Disemba 1 – Siku ya Ukimwi Duniani – wengi huangalia mapambano dhidi ya moja ya majanga yenye maangamizi zaidi katika historia.

Dkt. Chloe Orkin, wa Chuo Kikuu cha Queen Mary London anasema :"Hali ya ulimwengu inafungamana zaidi sana na pande za wale waliokuwa nacho na wale wasiokuwa na chochote. Kwa wale watu wanaoishi pale ambapo matibabu sio bure, au matibabu ni ya kizamani, matibabu yenye matatizo mengi ya kiafya, watu hawako katika hali nzuri. Na bila matibabu, HIV imeendelea kuwa ni maradhi yanayouwa watu.”

Wataalam wanasema matibabu yeye ufanisi yanazuia watu wenye maambukizi ya HIV kuambukiza virusi hivyo. Wanasema pia ulimwenguni kote, zaidi ya asilimia 50 ya wale wanaoishi na HIV ni wanawake, huku wanawake milioni 1.3 wenye HIV watakuwa wajawazito. Matibabu sahihi yanaweza kuzuia maambukizi ya virusi kwa mtoto aliyekuwa bado hajazaliwa.

Dkt Orkin wa Uingereza aliongoza juhudi za kimataifa kutengeneza tiba ya kwanza ya muda mrefu ya HIV. Anasema matibabu kama vile sindano anazopigwa mtu mara moja kila miezi miwili, zinapatikana.

Where I live, it could amount to six treatment days a year for someone with HIV, and that’s very different from having to take treatment 365 days a year. So, it’s a real breakthrough."

“Pale ninapoishi, inaweza kujumuisha siku sita za matibabu kwa mwaka kwa yule mwenye HIV, na hiyo ni tofauti na mtu kutakiwa kupata matibabu siku 365 kwa mwaka. Kwa hakika ni ushindi hasa.”

Watafiti wanafuatilia tiba kwa kuwachunguza wagonjwa wa HIV ambao mifumo yao ya kinga inapambana na HIV bila ya dawa.

Dkt Bruce Walker, Mkurugenzi wa Chuo cha Ragon anasema :

"Imethibitika kuwa baadhi ya watu wanaweza kudhibiti HIV kwa kutumia mifumo ya kinga za mwili wao, na hilo limetusukuma katika mwelekeo wa kujaribu kufahamu vipi hilo limewezekana.”

Loreen Willenberg ni mmoja wa wagonjwa wa namna hiyo. Aligunduliwa na maambukizi ya HIV mwaka 1992 lakini hajawahi kuwa na dalili zozote za maambukizi.

Willenberg, mgonjwa wa HIV anasema : Katika kipindi cha miaka 29 na nusu sijahitaji kutumia dawa za HIV. Nanyenyekea, na kushukuru.

Dkt Walker na wenzake wa Chuo cha Ragon wanafikiri itawezekana siku moja kuwatibu wale walioambukizwa na HIV.

XS
SM
MD
LG