Maafisa wa usalama nchini Sierra Leone wanapanga kufanya msako wa nyumba kwa nyumba kote katika mji mkuu wa Freetown kuwakamata wagonjwa wa Ebola waliojificha.
Freetown imekuwa kituo cha mlipuko wa ugonjwa wa Ebola ambapo iliripoti zaidi ya kesi mpya 130 katika wiki ya kwanza ya Disemba , ikiwa ni theluthi moja ya nchi nzima.
Katika taarifa yake rais wa Sierra Leone Bai Koroma aliwaambia wakazi wa Freetown wasiwafiche watu wanaougua Ebola wakati wafanyakazi wa afya walipoanza kutembelea nyumba hizo Jumanne.
Taarifa hiyo inasema msako huo una lengo la kupata kila mgonjwa ili kudhibiti kusambaa kwa virusi vya Ebola.