Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:35

Shule za kenya zafunguliwa rasmi 2013


Wanafunzi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, Kenya
Wanafunzi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, Kenya
Shule zimefunguliwa tena nchini Kenya kwa muhula wa kwanza wa masomo mwaka huu wa 2013 lakini katika jimbo la Tana River kulikotokea ghasia za kikabila na mauaji ya watu wengi huenda wanafunzi wengi wakakosa kurejea shuleni.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:45 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Maelfu ya watu katika sehemu hiyo ya Pwani ya Kenya wangali wanaishi kama wakimbizi wa ndani-IDP wakiwemo wanafunzi.

Awali kulikuwa na Wakimbizi wa ndani wapatao elfu 30 waliotoroka machafuko hayo, na japo idadi hiyo ilipungua bado kuna waliosalia katika Kambi hizo za muda.

Machafuko yalikumba Tana Delta tangu Agosti mwaka jana lakini wahanga walitorokea wilaya jirani za Malindi, Magarini, Kilifi, na Lamu Mashariki.

Kutokana na hali hiyo mwenyekiti wa muungano wa Riketa,Kilelengwani IDP Group, Abdalla Sanke huko Lamu Mashariki, anasema hofu kubwa ni kukosa nafasi za wanafunzi-wakimbizi, kuingia katika shule za karibu, na ukosefu wa ada ya shule.

Katika wilaya ya Magarini kuna wahanga wapatao 2,500 kutoka Tana Delta, na sasa shirika la msalaba mwekundu nchini humo limezindua mpango wa siku tatu wa kuwasajili wakimbizi halali, na idadi ya wanafunzi wanaoweza kuendelea na masomo.
XS
SM
MD
LG