Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 16:28

Shughuli za uokozi zaendelea Cambodia kufuatia mkasa wa moto kwenye Casino


Hoteli iliyochomeka moto kwenye mji wa Poipet, magharibi mwa mji mkuu wa Phnom Penh, Cambodia, Dec. 30, 2022.
Hoteli iliyochomeka moto kwenye mji wa Poipet, magharibi mwa mji mkuu wa Phnom Penh, Cambodia, Dec. 30, 2022.

Timu za waokozi nchini Cambodia Ijumaa zimendelea kutafuta manusura kwenye mabaki ya hoteli na Casino wakati idadi ya vifo kutokana na moto uliyolazimisha baadhi ya watu kurura kutoka kwenye madirisha ikifikia 25.

Mamia ya watu wanaaminika kuwa ndani ya hoteli hiyo ya Grand Diamond City, kwenye mji wa Poipet karibu na mpaka wa Thailand, pale moto ulipozuka usiku wa kuamkia Alhamisi.

Picha zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha watu wakiwa kwenye madirisha pamoja na paa la jengo hilo wakijaribu kuokoa maisha yao. Afisaa mmoja wa polisi wa Cambodia ameambia shirika la habari la AFP kwamba inaaminika kuwa watu wengi wamekwama ndani ya jengo hilo, huku waokozi wakiendelea kuwasaka.

Mamia ya wanajeshi , polisi pamoja na watu wa kujitolea wapo kwenye eneo la tukio wakiendelea na shuguli za uokozi. Ripoti zimeongeza kusema kwamba moshi uliendelea kutoka kwenye jengo hilo mapema Ijumaa, huku magari ya kuzima moto yakibaki chonjo. Wengi wa waliojeruhiwa wamepelekwa Thailand kwa matibabu wakati 13 miongoni mwao wakisemekana kuwa kwenye hali mahututi.

XS
SM
MD
LG