Shughuli za uokoaji kwa njia ya ndege zinatarajiwa kuanza Alhamisi kuwahamisha wakaazi katika mji mkuu wa jimbo la kaskazini magharibi mwa Canada kutoka kwenye njia ya moto wa msituni ambao ulikaribia mji huo wenye watu 20,000.
Watu katika maeneo manne ya Yellowknife walio katika hatari kubwa zaidi wanapaswa kuondoka haraka iwezekanavyo na wakazi katika maeneo mengine wana hadi saa sita mchana Ijumaa kuondoka katika eneo, serikali ya Northwest Territories ilisema.
Wale tu ambao hawana fursa ya kuondoka kwa njia ya barabara ndio wanaopaswa kujiandikisha kwa safari za ndege maafisa waliongeza. Watu ambao wana kinga dhaifu kiafya au wana hali inayowaweka katika hatari kubwa walihimizwa kujiandikisha.
"Nataka kuweka wazi kwamba mji huo hauko katika hatari kihivyo, na kuna muda salama kwa wakazi kuondoka kwenye mji kwa njia ya barabara na kwa ndege", Shane Thompson, waziri wa serikali za majimbo aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.
Moto huo ulikuwa unawaka kiasi cha kilomita 17 nje ya mji huo. Amri ya kuwahamisha watu iliyotolewa Jumatano usiku inatumika kwa mji wa Yellowknife na jamii jirani za Ndilo na Dettah zilizo katika First Nations.
Forum