Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 20:39

Shughuli kwenye uwanja wa ndege wa Damascus, Syria, zarejeshwa baada ya shambulizi la Israel


Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Damascus, Syria
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Damascus, Syria

Kundi la kutetea  haki za binadamu la Syrian Obsrevatory for Human Rights  limesema kwamba uwanja wa ndege wa kimataifa wa Damascus umefunguliwa tena baada ya kufungwa kwa muda kufuatia mashambulizi ya mizinga ya Israel kwenye mji huo mkuu wa Syria yaliouwa watu wanne wakiwemo wanajeshi wawili.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, hii ni mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miezi saba kushambuliwa na Israel. Makundi ya wapiganaji yanayoungwa mkono na Iran pamoja na wapiganaji wa Hezbollah wanashikilia udhibiti wa uwanja huo.

Mkuu wa kundi hilo Rami Abdul amesema kwamba silaha za Israel zililenga maeneo yanayokaliwa na Hezbollah pamoja na makundi yanyoungwa mkono na Iran ndani ya uwanja huo likiwemo ghala la kuhifadhia silaha. Wizara ya uchukuzi ya Syria imesema kwamba shughuli za kawaida zimerejeshwa baada ya kurekebishwa kwa baadhi ya maeneo yalioharibiwa.

Jeshi la Israel halijatoa tamko kuhusiana na tukio hilo, ingawa mara kadhaa limesema kwamba halitaruhusu hasimu wake Iran kueneza ushawishi wake nchini Syria.

XS
SM
MD
LG