Msemaji wa ICRC Diogo Alcantara nchini Afghanistan amesema ingawa wanaendelea kushauriana na wizara za serikali, wafadhili pamoja na mashirika ya kimataifa kubuni mikakati mbadala ya kuendesha sekta ya afya, program hiyo maalum ya Hospitali inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi Agosti.
Amesema kwamba ICRC haina mamlaka wala rasilimali za kuendesha mfumo mzima wa afya kwa muda mrefu nchini humo.
Mwezi Aprili bodi ya ICRC iliidhinisha msaada wa dola milioni 475.30 zikilenga kupunguza gharama ya huduma za kimatibabu mwaka huu na mwaka ujao, pamoja na kupunguza operesheni katika baadhi ya vituo kutokana na matarajio kwamba bajeti za misaada ya kibinadamu zingepungua.
Kumalizika kwa progam hiyo kunatokea wakati kuna wasi wasi kutokana na kupunguzwa kwa misaada mingine ya kibinadamu nchini Afghanistan, miaka miwili baada ya Taliban kuchukua madaraka.
Misaada mingine ya kimataifa ambayo ilikuwa imeshikilia uchumi wa taifa hilo ilisitishwa kuanzia wakati huo.
Forum