Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 14:04

Wanasiasa Marekani wavutaka kuhusu bunduki


Wajumbe wa baraza la Congress
Wajumbe wa baraza la Congress

Imekuwa ni muda wa wiki mbili tangu shambulizi baya zaidi la bunduki kuwahi kutokea Marekani.

Licha ya shinikizo kutoka kwa umma la kuimarisha sheria za umiliki wa bunduki, wajumbe wa baraza la Congress wangali wanavutana huku wajumbe wa kutoka chama cha Demokrat wakitumia mbinu zilizotumika miaka ya 60 kueleza kughadhabika kwao.

Umma vile vile umegawanyika hata baada ya shambulizi hilo la Orlando lililofanyika kwenye klabu.

Kura ya maoni ilofannywa na shirika la habari la CNN zinaonesha asilimia 55 ya Wamarekani wanaunga mkono sheria kali za umiliki wa bunduki.

Asilimia 57 wanaunga mkono kupigwa marufuku kwa bunduki kama iliotumika Orlando kulingana na takwimu zilizochukuliwa na shirika la habari la CBS.

Wengi wanalaumu kundi linalotetea haki za watengeneza bunduki.

XS
SM
MD
LG