Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 06:02

Sheria ya uhalifu na chuki inaipa idara ya polisi Marekani nguvu zaidi katika utendaji kazi


Baadhi ya wabunge wa Marekani wakielezea suala la uhalifu wa chuki Marekani sio la kufumbiwa macho

sheria hiyo inachukua lengo pana kwa uhalifu wote wa chuki, kwa kutoa wito wa kuteuliwa kwa afisa mpya wa idara ya sheria ili kuhakikisha ukaguzi wa kesi za uhalifu wa chuki na kutoa rasilimali kwa idara za polisi katika eneo ili kuboresha njia za kutambua na kuripoti uhalifu wa chuki

Mswaada uliopitishwa hivi karibuni uliosainiwa kuwa sheria na Rais Joe Biden hapo Alhamis unawapa maafisa wa kaunti na serikali kuu zana mpya na rasilimali za kupambana na uhalifu wa chuki huku ikiangazia ongezeko kubwa la chuki dhidi ya wa Asia wakati wa janga la COVID-19.

Msukumo wa sheria hiyo mpya inayojulikana kama “sheria ya uhalifu wa chuki katika COVID-19” kufuatia ongezeko kubwa la mashambulizi kwa wamarekani wenye asili ya Asia, tangu kuanza kwa janga hili huko Wuhan nchini China, zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Uhalifu wa chuki dhidi ya wa Asia katika miji mikubwa ya Marekani na kaunti zake uliongezeka kiasi cha asilimia 150 mwaka jana na mwaka mmoja kabla,na asilimia 194 wakati wa robo ya kwanza ya mwaka 2021 ikilinganishwa na robo ya kwanza ya mwaka 2020, kulingana na kituo kinachofuatilia masuala ya chuki na uhasama, kwenye chuo kikuu cha jimbo la California, San Bernardino.

Wakati ikionyesha ghasia dhidi ya wamarekani wenye asili ya Asia, sheria inachukua lengo pana kwa uhalifu wote wa chuki, kwa kutoa wito wa kuteuliwa kwa afisa mpya wa idara ya sheria ili kuhakikisha ukaguzi wa kesi za uhalifu wa chuki na kutoa rasilimali kwa idara za polisi katika eneo ili kuboresha njia za kutambua na kuripoti uhalifu wa chuki.

Mwanasheria mkuu wa Marekani, Merrick Garland akiwa Washington, D.C., April 21, 2021.
Mwanasheria mkuu wa Marekani, Merrick Garland akiwa Washington, D.C., April 21, 2021.

Sheria hii mpya itasaidia kuharakisha majibu yetu kwa uhalifu wa chuki na kutoa rasilimali kwa idara ya polisi kuboresha taarifa za uhalifu wa chuki zinazoripotiwa, alisema mwanasheria mkuu wa Marekani Merrick Garland katika taarifa yake. Sheria itasaidia idara ya polisi katika kulenga juhudi zake ambazo zitasaidia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG