Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 02:21

Sheria ya kuwavua madaraka Wabunge yapita Israel


Bunge la Israel Jumatano limepitisha sheria inayowawezesha wabunge kuwavua wadhifa huo wabunge wenzao ambao wanaochochea ghasia ubaguzi wa rangi.

Kutokana na kupita kwa sheria hiyo wakosoaji wameingiwa na hofu kwamba inaweza kutumika kuwalenga wabunge Waarabu.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, mbunge yoyote ambaye anachochea ubaguzi wa rangi ama kuunga mkono harakati za kutumia silaha dhidi ya dola la Israel, anaweza akaondolea ndani ya Bunge.

Sheria hiyo ilipita kwa ushindi mdogo wa kura 62 za ndio dhidi ya kura 47 za hapana.

Sheria hiyo itakapoanza rasmi, itahitaji kura 90 katika Bunge lenye wabunge 120 kuweza kumvua madaraka mbenge.

XS
SM
MD
LG