Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 05:35

Sherehe za Eid al Fitr zakumbwa na milipuko Nigeria


Sherehe za Eid al-Fitr zimekumbwa na milipuko ya mabomu huko Damaturu, Nigeria
Sherehe za Eid al-Fitr zimekumbwa na milipuko ya mabomu huko Damaturu, Nigeria

Milipuko zaidi ya mabomu imevuruga sherehe za Eid al-Fitr huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria na kuuwa watu wasiopungua 10 katika mji wa Damaturu.

Milipuko miwili ilitokea kwenye eneo la wazi ambapo waumini walikuwa wakisali katika siku ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhan. Baadhi ya ripoti zinasema kulikuwa na mlipuko mwingine uliofuatia baada ya milipuko hiyo miwili. Hakuna mtu yeyote anayedai kuhusika na mashambulizi, ambayo yametokea baada ya milipuko miwili katika mji wa Gombe hapo Alhamis.

Watu wasiopungua 50 waliripotiwa kuuwawa katika shambulizi hilo kwenye soko lililojaa wateja wakinunua bidhaa dakika za mwisho kwenye mkesha wa sikukuu ya Eid al-Fitr ambayo huadhimishwa kwa kukamilika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

XS
SM
MD
LG