Sharif alipata kura 174, ni mara mbili zaidi ya kura zilizokuwa zinahitajika ili achaguliwe na bunge la taifa lenye wabunge 342. Baadaye alikula kiapo, zoezi lililosimamiwa na kaimu Rais Sadiq Sanjrani.
Waziri mkuu huyo mwenye umri wa miaka 70 alichaguliwa na muungano wa vyama vya upinzani baada ya wabunge wa chama cha Khan cha PTI kususia zoezi la upigaji kura na kuondoka bungeni, wakiishtumu Marekani kuhusika katika kuiondoa serikali ya Khan.
Lakini Washington imetupilia mbali shutuma hizo, ikisema hazina ukweli wowote. Hata upinzani wa Pakistan umetupilia mbali shutuma hizo.
Dakika chache kabla ya kura hiyo, wabunge wa chama cha PTI walijiuzulu kwa pamoja.
Iwapo kujiuzulu kwa wabunge hao kutakubaliwa, kutahitajika uchaguzi mdogo kuhusu zaidi ya viti 100.