Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 11, 2023 Local time: 04:58

Miili ya Wajapan waliokufa Bangladesh kwa shambulio la ugaidi yarudishwa


Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Fumio Kishida, amesema leo Jumanne kwamba alishikwa na huzuni mno wakati miili ya raia saba wa Japan waliouwawa katika shambulizi kwenye mgahawa nchini Bangladesh iliporejeshwa nyumbani.

Waathirika hao walikuwa miongoni mwa mateka 20 na maafisa polisi wawili waliouwawa Jumamosi, mjini Dhaka.

Kishida alisema ni maumivu makali kwamba tumepoteza maisha ya watu kutokana na ukatili na ugaidi ambao ulipelekea haya yote kutokea. Aliahidi kwamba Japan itafanya kazi na jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kwamba shambulizi kama hilo halitatokea tena.

Maafisa wa Usalama wa Bangladesh awali walisema maafisa sita waliuwawa na walimkamata mmoja wao ambaye alifanya shambulizi. Lakini Ofisa Polisi Mwandamizi, Saiful Islam, alisema leo kwamba mmoja kati ya hao waliouwawa huwenda alikuwa mateka ambaye alifanya kazi katika mgahawa huo.

XS
SM
MD
LG